AMIR KHAN ARUDI ULINGONI KWA TKO YA MAPEMA




Baada ya kupotea na kuwa nje ya ulingo wa masumbwi kwa miaka miwili mfululizo, hapo jana bondia Mwingereza Amir Khan alirudi ulingoni na kumdunda kwa KO, Phil Lo Greco kutoka Kanada.

Mchezo huo wa ndondi uliopigwa katika ukumbi wa Liverpool Echo Arena ulimuacha Phil Lo Greco asijue la kufanya ndani ya sekunde 40 za mchezo huo.

Ni kama vile Khan alikua nje ya ulingo kufanya ngumi zake kuwa za moto zaidi kiasi kwamba makonde machache tu baada ya kengele ya kuashiria mchezo kuanza, yalimfanya Phil Lo Greco kwenda chini mara mbili kwa kusalimu amri na kumuonyeshea refa kwamba, imetosha na siwezi kuendelea kupokea kipigo hiki.

"Nimekuja ukumbini kufanya kazi nzuri na nataka kuwashukuru mashabiki wote''.
"Jose Gossen (kocha wake) alinambia "Usiende kutafuta knockout, lakini niliona nafasi na kuitumia." 

'Nilikua na wasiwasi wa kurudi Liverpool, baada ya miaka miwili, lakini nini? Nimekuja na kushinda!'

'Nimekuja kuwaonyesha mimi ni nani. Nataka kupambana katika mapigano bora na kuwa bingwa wa dunia tena.' 

Alisema Amir Khan kwa majigambo ndani ya ukumbi huo mbele ya mashabiki 9000 waliohudhuria pambano hilo.

 Amir Iqbal Khan amewahi kushikilia taji la dunia la uzito mwepesi, akishikilia WBA kutokea mwaka 2009-2012 na taji la IBF kwa mwaka 2011. WBC uzito wa Silva aliloshikilia mwaka 2014-2016.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.