KAMBI YA UGANDA YANOGA NGOMA AKIANZA RASMI MAZOEZI....




Straika mpya wa klabu ya Azam FC, ameanza mazoezi huko Uganda ambapo timu hiyo imeweka kambi ya wiki mbili hadi mwezi wa 8 tarehe 15.

Ngoma ameanza mazoezi mepesi kufuatua ushauri wa daktari wake juu majeruhi aliyonayo ili kujiweka fiti taratibu kuelekea dirisha la ligi kufunguliwa Agosti 22.

Ikimbukwe nGoma alipewa mapumziko ya wiki tisa baada ya kugundulika ana uvimbe kwenye goti lake la kulia ikiwa ni baada ya kufanyiwa vipimo vya afya katika hospitali ya St. Vincent Parrot iliyoko Afrika Kusini.

Taarifa kutoka Azam zinaeleza hali ya Ngoma kwa sasa inaendelea vizuri japo bado hajaimarika kisawasawa ingawa matumanini ya kupona kwake yapo kwa siku za usoni.

Azam inatarajiwa kurejea nchini baada ya wiki ijayo tayari kwa maandalizi ya mwisho kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.