Baada
ya Mfaransa, Patrick Liewig kuachana na Stand United, sasa imeelezwa
mikoba yake itachukuliwa na Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco
ambaye tayari ameshafanya mazungumzo ya awali na uongozi wa klabu hiyo.
Morocco
ambaye amewahi kuzinoa Coastal Union na Timu ya Taifa ya Zanzibar,
ataungana na Athuman Bilal ‘Bilo’ katika kuiongoza timu hiyo inayoshika
nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Kwa
mujibu wa katibu wa klabu hiyo, Kennedy Nyangi, ni kwamba, baada ya
kuwa na mazungumzo na makocha wengi, lakini wamefikia maamuzi ya kukaa
chini na kumalizana na kocha huyo.
“Tulikuwa
na mazungumzo na makocha wengi ili kuziba nafasi ya Liewig, kati ya hao
tumeona Hemed Morocco anafaa kuwa kocha wetu mkuu, kilichobaki kwa sasa
ni kuona ni kwa namna gani tunamalizana naye,” alisema Nyangi.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.