Kiungo
mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, amewaambia Simba kwamba mzunguko wa
pili wa Ligi Kuu Bara wasahau kabisa kutesa kama ilivyokuwa mzunguko wa
kwanza.
Msuva
ambaye mpaka sasa ana mabao saba katika ligi hiyo, ameisaidia Yanga
kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 33 nyuma ya Simba yenye 35,
huku timu hizo zote zikipoteza michezo miwili mpaka sasa.
Msuva
ameliambia gazeti hili kuwa, mzunguko wa pili watafanya jitihada zote
kuhakikisha wanaipindua Simba kwenye nafasi hiyo na kuikamata wao mpaka
mwisho wa msimu.
“Simba
wamekaa nafasi yetu na nawaambia mzunguko wa pili tutafanya kila
liwezekanalo kuhakikisha tunawatoa hapo, tukikaa sisi hatutoki mpaka
msimu unamalizika kwani tumedhamiria kuutetea ubingwa wetu,” alisema
Msuva ambaye ni Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara mwezi Oktoba.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.