Roberto Martinez: Kocha wa zamani Everton apewa kazi Ubelgiji



Image copyrightPA
Image captionMartinez aliwaongoza Wigan kushinda Kombe lao la kwanza kabisa la FA, kwa kuwalaza Manchester City katika fainali mwaka 2013
Meneja wa zamani wa Everton, Wigan na Swansea Roberto Martinez ameteuliwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji.
Martinez, 43, ambaye ni raia wa Uhispania, alifutwa kazi Everton mwezi Mei baada ya kufanya kazi Goodison Park kwa miaka mitatu.
Marc Wilmots alijiuzulu wadhifa wake kama meneja wa Ubelgiji mwezi jana, wiki mbili baada ya kushindwa na Wales robofainali michuano ya Euro 2016.
Nafasi yake ilitangazwa wazi mtandaoni na Shirikisho la Soka la Ubelgiji.
Shirikisho hilo lilisema linamtafuta mtu bingwa katika mawasiliano na mwenye uwazi na ambaye amethibitisha uzoefu katika kuwapa wachezaji nyota ujuzi na ustadi katika ufundi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.